Kala Tufaha

Hili fumbo kajifumbia mwenyewe Fumbwe. Kamlisha mwana wa watu tufaha na kumsaliti mkewe Hatima. Tufaha kampata Kala hali Fumbwe katorokwa na Hatima. Malipo hapa hapa duniani; hatima ya Fumbwe ni kukutana na Daktari Kala Tufaha mwishoni mwa safari yake duniani baada ya kulionja tufaha lenye dudu.

Kala Tufaha ni hadithi ya kiistiari iliyomulika maovu na magandamizi wanayofanyiwa wanawake. Kibibi anakosa nafasi yake shule kutokana na jinsia yake. Anakoelekea kutafuta riziki bwanyenye linammezea mate. Mimba asiyoikusudia yamfanya kufukuzwa nyumbani. Lakini mwishowe kicheko kinakuwa chake na mwanaye Kala wanapoyaonja matokeo ya juhudi na ujasiri.

KES550.00

SKU: RGB9966472851 Categories: , , , ,
The Magunga Bookstore
Babu Omar (Abu Ashraf)

Omar Babu, akijulikana pia kama Abu Ashraf ama Abu Marjan, ni msomi na mwandishi wa Kiswahili wa kutajika. Amesomea viyuo vikuu vya Nairobi na Ohio State, Marekani, na kwa sasa ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Cologne, nchini Ujerumani.

Amewahi pia kuwa mtangazaji wa redio na televisheni, na ni mmoja wa washairi waliochangia mkusanyiko wa karibuni, Diwani ya Karne Mpya, ambao pia umechapishwa na Phoenix Publishers Limited.