Mizungu ya Manabii na Hadithi Nyingine

Hadithi fupi zimekuwa utanzu wa kuipigia darubini jamii ibuka. Katika mkusanyiko huu mna hadithi kumi na mbili zinazoangazia maswala yanayolikabili bara la Afrika katika karne ya ishirini na moja: ufisadi; mila-lemazi; ufukara; unyanyasaji wa uana, na kadhalika. Zote zimesukwa kitaalamu ili kutolea msomaji burudani na vilevile mafunzo muhimu kuihusu jamii yake.

KES400.00

The Magunga Bookstore
Dkt. John Habwe (mhariri na mwandishi)

Mhariri wa hadithi hizi, Dkt. John Habwe, ni mtaalamu wa Kiswahili na mhariri katika idara ya Isimu na Lugha za Kiafrika, Chuo Kikuu cha Nairobi. Vilevile yeye ni mwandishi was kutajika ambaye amechapisha riwaya, hadithi fupi, makala ya kitaaluma na vitabu vya kufunzia lugha.